Michezo

Kocha wa Man City kawapa habari njema FC Barcelona kuhusu Griezmann

on

Baada ya kutangaza kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Antoine Griezmann anaondoka Atletico Madrid mwisho wa msimu wa 2018/2019, wengi wanataka kufahamu staa huyo ataenda timu gani msimu ujao japokuwa kwa sasa anahusishwa sana na FC Barcelona.

Barcelona wanadaiwa kumuhitaji Griezmann mwenye umri wa miaka 28 ila inadaiwa Man City wanaweza wakawa na nia nae ya chini kwa chini, hivyo wawe makini wasije kupigwa bao, kocha wa Man City ambaye amewahi kuichezea na kuifundisha FC Barcelona Pep Guardiola amewatoa hofu Barcelona.

“Kwa watu wa FC Barcelona nilisema msijali jamani, Man City haitomsajili Antoine Griezmann,bei yake hatuwezi kuimudu”>>> Kocha wa Man City Pep Guardiola

FC Barcelona wametenga euro milioni 125 kukamilisha usajili huo, Griezmann amekuwa nguzo muhimu ya ushambuliaji ya Atletico Madrid toka 2014 alipojiunga nayo akitokea Real Sociedad ya nchini humo, Griezmann mwenye umri wa miaka 28 kwa sasa inaelezwa atapewa mkataba wa miaka mitano na FC Barcelona.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments