Michezo

Arsenal watoa kipigo nje ndani kwa Napoli, sasa waungana na Chelsea nusu fainali

on

Club ya Arsenal ya England wakati ikiwa inaaminika kuwa ilikuwa na mshindani imara katika michuano ya UEFA Europa League hatua ya robo fainali kwa kupangwa na Napoli, leo imewadhiirishia umma kuwa ina uwezo wa kupambana na yoyote na kupata matokeo.

Kutokana na mwenendo ambao sio mzuri sana  wa Arsenal katika Ligi, pamoja na kupata ushindi wa magoli 2-0 katika mchezo wao wa kwanza katika uwanja wao wa Emirates, wengi walitarajia kuona Napoli inapindua matokeo ikiwa nyumbani kwao kitu ambao kimekuwa tofauti na wamejikuta wakipokea kipigo nje ndani yaani nyumbani na ugenini.

Baada ya Alexander Lacazette kuifungia Arsenal goli la ushindi 1-0 dakika ya 36 dhidi ya Napoli, Arsenal sasa wanakuwa wameiondoa Napoli kwa ushindi wa jumla ya magoli 3-0, hivyo Arsenal wanaungana na majirani zao wa jiji la London club ya Chelsea kucheza nusu fainali sambamba na Frunkfurt na Valencia.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments