Top Stories

Mwili uliozikwa mwezi mmoja uliopita, wafukuliwa Moshi

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro imeamuru kaburi la Juma Hamis Juma lifukuliwe na mwili wake upimwe na majibu ya vipimo hivyo yaambatanishwe kwenye ushahidi.

Juma Hamis alifariki na kuzikwa mwezi mmoja uliopita baada ya kupigwa na watu na kusababisha kifo chake lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida alizikwa bila mwili wake kuchukuliwa vipimo.

Baba mdogo wa marehemu, Salim Juma Abdallah amesema marehemu alivamiwa na kupigwa na watu ambao sasa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo baada ya kupigwa alipoteza fahamu na alibaki katika hali hiyo hadi alipofikwa na umauti ambapo alizikwa bila kufanyiwa vipimo lakini Mahakama imeelekeza mwili wake ufukuliwe na upimwe kisha majibu ya vipimo viambatanishwe kwenye ushahidi.

HUZUNI HARUSINI!!! Mabwana harusi waugua baada ya kula chakula chenye sumu

Soma na hizi

Tupia Comments