Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

VIDEO: TFF wametoa baraka kwa Waandishi wa Michezo wanaoisapoti Taifa Stars kwenda CHAN

on

Shirikisho la soka Tanzania TFF leo kupitia katibu mkuu wake Wilfred Kidau limetangaza rasmi kuwaunga mkono kwa vitendo waandishi wa habari za michezo 30 waliojitolewa kuhamasisha Taifa Stars ishinde kwa ajili ya kufuzu kucheza CHAN 2020 nchini Cameroon.

TFF imeonesha kwa vitendo kusapoti waandishi hao na tayari imeahidi kutoa basi la kuwasafirisha waandishi hao na kuwachangia Tsh Milioni 2 kwa ajili ya safari ya kuelekea jijini Nairobi Kenya katika mchezo wa marudiano dhidi ya Harambee Stars.

Taifa Stars ya wachezaji wa ndani nchini Kenya kwenye mchezo wa marudiano watalazimika kutafuta ushindi au sare ya kufungana magoli ili kusonga mbele na kuitoa Kenya, hiyo inatokana na mchezo wao wa kwanza uwanja wa Taifa kumalizika kwa sare tasa (0-0).

VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6

Soma na hizi

Tupia Comments