Rais wa @gsmgroupofcompanies mdhamini na mfadhili wa klabu ya Yanga Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ akiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa hii leo amechangia Tsh milioni 60 kwa ajili ya maboresho ya kituo cha Afya cha Kibaigwa.
GSM Ameahidi kisima cha maji, lakini pia ametoa mashine ya kuhudumia watoto njiti na matengenezo ya sehemu maalumu ya kupumzikia au kusubiria wakati wa kutoa huduma.