Michezo

GSM amkaribisha Manji Yanga “tuungane”

on

Mchambuzi wa habari za soka kutoka Clouds FM Privaldinho alipata nafasi ya kukutana na mdhamini na mfadhili wa Yanga SC Ghalib Said Mohammed na kufanya nae mazungumzo, kubwa kumuuliza kuhusiana na tetesi za kurejea Yanga kwa aliyekuwa mfadhili wa Yanga wakati huo Yussuf Manji.

Ghalib Said Mohamed (GSM)

Privaldinho : “Umesikia habari za Manji kurejea Yanga?”

GSM: “Naam, nimezisikia. Binafsi nitafarijika sana akirudi. Ujio wake utakuwa msaada thabiti Yanga. Sio Manji tu, yeyote mwenye nia ya dhati ya kuisaidia aje tuungane kwa pamoja. Mshikamano huleta maendeleo maradufu” 

Manji

Yanga SC kwa sasa chini ya kampuni ya GSM ambao ndio kampuni yao inaowadhamini katika vifaa vya michezo, imejitolea pia kuhakikisha mfumo wa mabadiliko YangaSC unakamilika kwa ufasahau sambamba na kufuata ushauri wa kitaalam.

Soma na hizi

Tupia Comments