Michezo

DoneDEAL: Chelsea wamemalizana na Maurizio Sarri kujiunga Juventus

on

Club ya Chelsea ya England leo imetangaza rasmi kuwa aliyekuwa kocha wao Maurizio Sarri kaihama club hiyo na kujiunga na club ya Juventus ya Italia, Sarri anarudi Italia kuijunga na Juventus kwa mkataba wa miaka mitatu, hiyo ni baada ya kuifundisha Chelsea kwa msimu mmoja pekee.

Kocha Maurizio Sarri amejiunga na Juventus akitokea Chelsea, Sarri anaondoka Chelsea akiwa kaisaidia kutwaa taji moja la UEFA Europa League 2018/19 na kuvunja rekodi yake ya kukaa miaka 11 bila taji lolote akiwa kafundisha vilabu 7.

Moja kati ya sifa ambazo Chelsea watamkumbuka Sarri ni pamoja na kuisaidia timu hiyo kupata nafasi ya kucheza UEFA Champions League kwa msimu wa 2019/2020, hata hivyo aliifikisha pia Chelsea fainali ya Capital One Cup na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa na Man City.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments