Top Stories

Tamko la CHADEMA baada ya Ofisi za Mawakili kuvamiwa leo

on

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kimesema kimepokea kwa masikitiko taarifa za kuvamiwa kwa Ofisi za Kampuni ya Mawakili wa Kujitegemea IMMMA Advocates na kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema Chama hicho kinafahamu kwa mujibu wa Mikataba ya Kimataifa, Mawakili wana haki ya kufanya kazi zao kwa uhuru na faragha wakati wa kutoa huduma zao kwa wateja wao na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Mrema amesema kuwa Chama hicho kinatoa rai kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kutoa taarifa kwa umma ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wahusika wanapelekwa kwenye vyombo vya Sheria.

Aidha, Mrema amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mawakili (The Advocates Act) Mawakili ni Maafisa wa Mahakama ambao huisaidia Mahakama katika kutenda haki, hivyo chama hicho wanaona hilo ni shambulio dhidi ya Mahakama kwa kuwa maafisa wake wameshambuliwa.

ULIPITWA? Ofisi ya Wakili Fatma Karume yateketea, kinachodaiwa kuwa chanzo chatajwa…tazama kwenye hii video!!!

Play kwenye hii video hapa chini kutazama Mlinzi akisimulia kilichotokea usiku kabla jengo la Mawakili kulipuliwa… 

Soma na hizi

Tupia Comments