Michezo

RC Makonda kaamua kumpa zawadi ya heshima Samatta

on

Kama utakuwa unakumbuka vizuri wakati wa utoaji wa Tuzo za MO Simba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliahidi kuwa kila mchezaji wa Simba aliyeshinda tuzo atampatia zawadi ya Tsh milioni 1 ila golikipa wa Simba SC Aishi Manula aliyeisaidia sana Simba katika mchezo wa ugenini dhidi ya TP Mazembe nchini Congo atampa Tsh Milioni 10.

Baada ya kumalizana na wachezaji wa Simba SC RC Paul Makonda kutokana na kuvutiwa na kufarijika na jitihada za Mbwana Samatta katika soka sambamba na kuitangaza Tanzania barani Ulaya akiichezea KRC Genk ikiwemo kuisaidia club hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu Ubelgiji kwa mara ya kwanza baada ya miaka 9.

RC Makonda ameamuahidi Mbwana Samatta kumpa mtaa wa viwango ambao atahita jina la Mbwana Samatta hiyo inatokana na heshima, huku akishauri wachezaji wa kitanzania kuwa kama Samatta kwa kufuata nyendo zake ambazo zimepelekea kuwa na heshima kubwa kwa taifa.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

 

Soma na hizi

Tupia Comments