Michezo

EXCLUSIVE: Shabani Iddi Chilunda amefunguka ishu ya kutolewa kwa mkopo Hispania

on

Staa wa Tanzania aliyejiunga na Club ya CD Tenerife ya Hispania August 2018 akitokea Azam FC, Shaban Iddi Chilunda ameripotiwa kutolewa kwa mkopo na club yake hiyo na kwenda katika club ya CD Izarra ya Hispania pia.

Chilunda mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na CD Tenerife August 2018 kwa mkataba wa miaka miwli na sasa ametolewa kwa mkopo wa miezi sita kwenda club ya CD Izarra, hivyo Tenerife wamempeleka huko ili apatae nafasi ya kucheza zaidi.

“Ni kweli naenda kwenye hiyo timu na naenda kwa sababu hapa sijapata nafasi ya kucheza toka nimefika hapa nikawaomba juzi nivunje mkataba niende Sweden kuna timu nilikuwa nimeipata ila wamekataa wakaniambia tatizo sio wao ni kocha ana wachezaji wake”>>>Chilunda

“Wakaniambia sisi hatuwezi kuvunja mkataba na wewe sisi tunakuhitaji basi mimi niruhusuni niende Sweden nikacheze kwa mkopo wakaniambia hawawezi kuniruhusu niende Sweden kwa sababu Ligi yao ni bora kuliko Sweden bora ucheze hapa tukuangalie ndio wamenitafutia CD Izarra ya daraja la pili”>>> Chilunda

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments