Michezo

Arsenal wamelalamikia kupewa tiketi 6000 mashabiki wake fainali ya Europa League

on

Moja kati ya michezo migumu kupata tiketi ni pamoja na michezo ya fainali za UEFA Champions League na UEFA Europa League, baada ya kufahamika kuwa timu za Arsenal na Chelsea ndio zitacheza fainali ya UEFA Europa League katika mji wa Baku katika uwanja wa Olympic wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 68700, zimetangazwa idadi ya tiketi watakazopewa.

Imetangazwa kuwa tiketi zitakazotolewa kwa ajili ya mashabiki wa Chelsea na Arsenal katika mchezo wa fainali ya Europa League May 29 2019 ni tiketi 6000 kwa kila timu, huku idadi iliyosalia kuuzwa kwa utaratibu wa kawaida, kupewa tiketi 6000 haina maana wanapewa bure ila watanunua sema watakuwa wamepewa kipaumbele mashabiki wa timu hizo kwa kiwango hicho.

Gharama ya tiketi ya kuangalia mchezo huo kwa tiketi moja itakuwa inaanzia kati ya pound 26 (Tsh 77,993) hadi pound 121 (Tsh 362,966), pamoja na hivyo Arsenal wamelalamikia kuwa idadi ya tiketi 6000 ni ndogo kwani idadi kubwa ya mashabiki wao watakosa kuangalia fainali ya michuano hiyo, ambayo timu yao itakuwa inacheza kwa mara ya kwanza fainali ya Ulaya tokeo 2006.

Samatta kaweka historia Ubelgiji, mchezaji wa tatu kuwahi kushinda Ebony Award 2019

Soma na hizi

Tupia Comments