Michezo

Simba SC baada ya Tsh bilioni 1.5 kutokana CAF wapokea na Tsh milioni 50

on

Baada ya shirikisho la soka Afrika CAF kuendeleza utamaduni wake wa kutoa Tsh Bilioni 1.5 kwa timu zote nane zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF Champions League, Simba SC ni miongoni mwa timu hizo nane watakaopewa Tsh Bilioni 1.5.

Kila hatua ya timu zinazofikia katika michuano ya CAF Champions League kuna kiasi cha pesa huwa wanapewa, hivyo kwa upande wa Simba SC wadhamini wao wakuu kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa nao imetangaza kuwa itawapa Tsh milioni 50.

Kiasi cha Tsh milioni 50 kitakachotolewa kwenda kwa Simba SC kinatokana na makubaliano ya kimkataba kati ya Simba SC na SportPesa ambapo Simba SC itakuwa inapewa pesa hizo kama zawadi kwa kufikia au kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika, hilo limethibitishwa na mkurugenzi wa utawala na utekelezaji wa SportPesa Abbas Tarimba.

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments