Michezo

Mama mzazi wa Rabiot alalamika PSG hakuna usawa, mwanae kama mfungwa

on

Mama mzazi (Veronique Rabiot) na wakala wa mchezaji wa Paris Saint Germain ya Ufaransa Andrien Rabiot wiki hii amegonga vichwa habari baada ya kutoa kauli ya kushangaza kidogo kwa madai ya kuwa mtoto wake akiwa katika club yake ya Paris Saint Germain ni kama mfungwa.

Veronique Rabiot amesema kuwa namna ambavyo anachukuliwa mwanae ni tofauti na wanavyochukuliwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, kitu ambacho ameweka wazi kuwa hafurahishwi nacho hata kidogo, mkataba wa Rabiot unamalizika mwisho wa msimu huu na ameweka wazi msimamo wake kuwa hatoendelea nao.

Uamuzi wa Rabiot kutoendelea kuichezea PSG umesababisha staa huyo atolewe katika list ya wachezaji wanaotakiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza, hata hivyo mama yake amelalamika kuwa mwanae na baadhi ya wachezaji hawapewi usawa na amekuwa akipendelea Neymar kufanya anachotaka kama sasa hivi ni majeruhi lakini alionekana katika matamasha ya usiku.

“Mwanangu ni kama mfungwa PSG kitu pekee alichoomba ni kumalizia mkataba wake, walimpiga faini kwa sababu ya kutosafiri na timu kwenda Qatar wakati ambao alikuwa kafiwa na bibi yake, PSG wamekuwa na utamaduni wa kuwapiga faini wachezaji wanaochelewa katika kikao kwa dakika 6 lakini wengine wakiwa majeruhi (Neymar) wanaruhusiwa kusafiri mahala popote duniani kuhudhuria matamasha”>>>>Veronique Rabiot

Kama utakuwa unakumbuka vizuri uongozi wa PSG uliwapiga faini ya euro 180000 Kyliane Mbappe na Andrien Rabiot kama sehemu ya kuwaadhibu na kuwapa onyo kufuatia kitendo chao cha uchelewaji katika kikao cha timu October 2018.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars.

Soma na hizi

Tupia Comments