Michezo

Hii ndio Super Sports FC aliyokwenda kufanya majaribio Gadiel Michael wa Yanga

on

Beki wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na club ya Yanga SC Gadiel Michael Mbaga ameondoka nchini leo kuelekea Afrika Kusini katika club ya Super Sports kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki mbili katika club hiyo yenye makazi yake Pretoria na inatumia uwanja wa nyumbani wa Lucas Moripe.

Mbaga ameondoka leo akiwa na baraka zote kutoka kwa uongozi wa club yake ya Yanga SC, kama Gadiel Michael atajiunga na Super Sport itakuwa ni fursa nzuri kwake na kwa taifa kutokana na Ligi ya Afrika Kusini kuwa juu,hata hivyo atakuwa anaungana na mtanzania mwenzake Abdi Banda anayecheza Ligi ya nchi hiyo akiwa na Baroka FC.

Gadiel Michael

Club ya Super Sports ni club inayomilikiwa na kampuni ya vituo vya TV vya Super Sports nchini Afrika Kusini na ilianzishwa 1994, msimu wa 2017/2018 timu hiyo ilimaliza nafasi ya 7 katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Afrika Kusini, msimu huu Super Sports ipo nafasi ya 5 ikiwa na point 39 tofauti ya point 4 dhidi ya Mamelod Sundowns wanaongoza Ligi .

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments