Baada ya kumalizika kwa michezo ya marudiano ya nusu fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 na kushuhudia timu za Liverpool na Tottenham za England zinaingia fainali ya UEFA Champions League, usiku wa May 9 2019 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia UEFA Europa League game za marudiano za nusu fainali Chelsea dhidi ya Frankfurt na Valencia dhidi ya Arsenal.
Arsenal wao wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-2 ugenini yaliofungwa na Pierre Aubameyang aliyefunga hat-trick dakika ya 17, 69 na 88 huku Lacazette akifunga la pili dakika ya 22, Valencia wakiishia kuambulia mawili yaliofungwa na Gameiro dakika ya 1 na 58, hivyo Valencia wakajikuta wametolewa katika michuano hiyo na Arsenal kuingia fainali kwa aggregate ya 7-3.
Chelsea mambo yalikuwa magumu baada ya sare 1-1 dakika 90 na ukiangalia na mchezo wa kwanza kuwa na sare ya 1-1, hivyo aggregate kuwa 2-2 ikalazimika dakika 120 zichezwe kupata mshindi ambapo mambo yalikuwa magumu na game kumalizika 1-1, goli la Chelsea likifungwa na Loftus-Cheek dakika ya 28 na Frankfurt lilifungwa na Jovic dakika ya 49, penati 4-3 zikaiondoa Frankfurt.
Kufuatia timu zote nne za England kufuzu fainali za Champions League na Europa League hii ndio inakuwa kwa mara ya kwanza kwa timu nne za taifa moja kufika fainali za michuano ya Ulaya katika msimu mmoja, huku timu tatu kati ya hizo zikitokea katika jiji la London Chelsea, Arsenal na Tottenham, game ya fainali ya Europa League itachezwa May 29 2019 katika mji wa Baku.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania