AyoTV

AFCON U-17 wametangaza maamuzi mapya, viingilio bure

on

Leo michuano ya AFCON U-17 2019 ndio imezinduliwa rasmi Tanzania ikiwa ndio mwenyeji wa michuano hiyo, pamoja na kuwa Tanzania imeanza vibaya kwa kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nigeria kwa magoli 5-4, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza kuwa serikali imeamua kufanya mashindano hayo bure bila kiingilio.

Agizo hilo la waziri mkuu Kassim Majaliwa limewekewa mkazo na waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo aliongea na waandishi wa habari na kuwekea mkazo kuwa mechi zote za michuano hiyo itakuwa bure.

Kutokea Algeria, Morocco na Hispania Ulimwengu, Msuva na Chilunda kuhusu Kundi C AFCON 2019

Soma na hizi

Tupia Comments