Michezo

Ronaldo De Lima amesema Lionel Messi nae anastahili kulaumiwa

on

Imekuwa ni hulka ya kawaida kwa mashabiki wa club ya FC Barcelona ya Hispania kupenda kumsifia Lionel Messi kuwa ndio amechangia ushindi au matokeo ya Barcelona pale ambapo timu hiyo inakuwa imepata matokeo chanya lakini imekuwa ni ngumu kwa mashabiki hao wa Barcelona kumsema vibaya Messi ikitokea timu hiyo ikapoteza mchezo.

Ronaldo

Staa wa zamani wa timu za Real Madrid na FC Barcelona zote za Hispania Ronaldo De Lima amefunguka na kuwalaumu mashabiki wenye kasumba ya utamaduni huo mbovu na klibaguzi, kama wanaona kuwa timu imepoteza ni vyema kuilaumu timu nzima kuliko kuwalaumu watu baadhi na kumtoa Messi ambaye yeye wamemuweka katika kipengele cha kumsifia tu.

Ernesto Valverde

“Baada ya Barcelona kupoteza siku iliyofuatia nikasikia kuwa makosa yalikuwa ya kocha wao (Ernesto) Valverde, Coutinho lakini kamwe sio makosa ya Messi badala yake ikitokea wakishinda inakuwa ni Barcelona ya Lionel Messi ndio imeshinda hiyo sio haki kwa wachezaji wote na benchi la ufundi”>>> Ronaldo De Lima

Ronaldo

Kama utakuwa unamkumbua vizuri Ronaldo De Lima raia wa Brazil hadi anastaafu soka alikuwa anatajwa kama mongoni mwa washambuliaji bora wa muda wote waliowahi kutokea katika soka na amewahi kuzichezea timu mbalimbali ikiwemo FC Barcelona, Inter Milan, Real Madrid, AC Milan na Corinthians ya kwao Brazil.

Samatta kaweka historia Ubelgiji, mchezaji wa tatu kuwahi kushinda Ebony Award 2019

Soma na hizi

Tupia Comments