Michezo

PICHA 10: Sevilla FC wameshatua Tanzania kuwapima Mabingwa Simba SC

on

Club ya Sevilla FC ya Hispania ambao wamewahi kuwa Mabingwa wa UEFA Europa League leo wamewasili Tanzania katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya kumaliza LaLiga, Sevilla wamewasili Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba SC May 23 2019.

Sevilla ndio itakuwa timu ya kwanza kuwapima nguvu Simba SC toka watangazwe kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara leo kwa mara ya pili mfululizo, hiyo ni baada ya game yao dhidi ya Singida United kumalizika kwa wao kupata ushindi wa magoli 2-0.

 

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments