Michezo

Esperance wapewa Ubingwa baada ya Wydad kugoma kuendelea kucheza

on

Game ya pili ya marudiano ya CAF Champions League kati ya wenyeji Esperance ya Tunisia dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco imechezwa mjini Rades, game hiyo imechezwa lakini imekuwa na matukio ya kushangazwa zaidi baada ya game hiyo kutofikia tamati ya dakika 90 kutokana na wachezaji wa Wydad kuharibu game.

Wachezaji wa Wydad Casablanca ndio wamesababisha game hiyo kushindwa kumalizika na matokeo yake kujikuta Esperancea wakitawazwa kuwa Mabingwa wa michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo, hadi game ya pili ya marudiano inaanza aggregate ilikuwa inasomeka 1-1.

Tatizo lilikuja kuanzia dakika ya 62 baada ya dakika Esperance kupata goli la kuongoza kupitia kwa Youcef lakini dakika ya 62 Walid akafunga goli la kuisawazishia Wydad lakini lilikataliwa kutokana na muamuzi kuonesha kibendera kuwa wameotea ndipo hapo balaaa lililopoanza na Wydad kuamini kuwa wanaonewa na kugomea kuendelea na mchezo huo.

Hata hivyo game hiyo imeonekana kuwashinda marefa wengi baada ya refa wa kwanza raia wa Misri aliyechezesha game ya kwanza kusimamishwa kwa miezi sita, kwa madai kuwa alichezesha akiwa chini ya kiwango, hivyo ilivyotokea leo ikawa rahisi kwa Wydad kuhisi wanaonewa hususani muamuzi hakwenda hata kuangalia VAR ili aweze kutengua au kuendelea na uamuzi wake.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments