Michezo

Cristiano Ronaldo amekubali kulipa Tsh Bilioni 50 ili kukwepa kwenda jela

on

Staa wa club ya Juventus ya Italia Criastiano Ronaldo leo mapema aliwasili Mahakamani Hispania akiwa na mpenzi wake kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi yake ya ukwepaji kodi nchini Hispania wakati akiichezea club ya Real Madrid ya Hispania.

Cristiano Ronaldo alikuwa na kesi ya ukwepaji kodi ya haki za picha zake na mapato yake ya nje ya uwanja kosa ambalo imeripotiwa alilitenda kati ya mwaka 2011 na 2014 akiitumikia Real Madrid ya Hispania, hivyo Ronaldo amehukumiwa kifungo cha miezi 23 jela au faini ya zaidi ya Tsh Bilioni 50.

Ronaldo amekubali kulipa faini hiyo lakini mchezaji mwenzake wa zamani Xabi Alonso yeye ameonekana Mahakamani pia na inatajwa kuwa akikutwa na hatia atafungwa miaka mitano jela, Ronaldo alihama Real Madrid mwaka 2017 na kujiunga na Juventus baada ya kudumu Real Madrid kwa miaka tisa.

Xabi Alonso

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments