AyoTV

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

on

Moja kati ya habari kubwa katika mitandao ya kijamii katika soka la bongo ni pamoja na tukio la Adam Salamba wa Simba baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Simba SC dhidi ya Sevilla ya Hispania kumfuata Ever Banega na kumuomba viatu vyake, unajua wengi wamezoea kuona wachezaji wakibadilishana jezi lakini baada ya Salamba kumuomba viatu Banega likawa gumzo.

AyoTV imempata mchezaji wa timu ya taifa ta Tanzania Taifa Stars na club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva baada ya kutua tu Airport leo, Msuva wewe umecheza game nyingi za kimataifa na club na timu ya taifa kitendo cha Salamba kumuomba viatu Ever Banega umekipokeaje.

“Kwangu mimi ni kitu cha kawaida kabisa hata kama ningekuwepo pengine ningeweza kuomba hata picha, sema wanaomsema watakuwa ni watu wanaoshabiki mpira hawajui mpira ila ni kitu cha kawaida kabisa ile pale ni kama kumbukumbu kwake”>>>Msuva

Mwacheni Salamba achukue viatu vya Ever Banega kwa ajili ya watoto wake

Soma na hizi

Tupia Comments