Michezo

DONE DEAL: Habib Kiyombo amesaini Mamelod Sundowns

on

November 29 2018 zilisambaa taarifa kuwa mshambuliaji wa club ya Singida United ya Singida Habib Kiyombo yupo mbioni kusaini mkataba wa kuitumikia club ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, taarifa zilikuwa zinaripoti kuwa ni muda wowote anasaini ila baadae ikawa kimya.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga alipokuwa akifanya mahojiano na Nyundo ya Baruan kupitia Azam TV amelithibitisha hilo “Leo Singida United inazungumzwa Minnesota Marekani, inazungumzwa Mamelod Sundowns kwa sababu sisi ndio timu ya kwanza kufanya biashara na Kaizer Chiefs, biashara ya Habib Kiyombi ilishafanyika na amesaini Mamelod mkataba wake unaanza June 2019”>>> Festo Sanga

Festo Sanga

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Habib Haji Kyombo aliyekuwa tishio katika kufumania nyavu, alijiunga na Singida United akitokea Mbao FC ya Mwanza mapema mwaka 2018, kama Habib amefanikiwa kusaini mkataba kama ilivyothibitisha atakuwa anaungana na mtanzania mwenzake Abdi Banda katika Ligi moja ya Afrika Kusini, Banda akiichezea Baroka FC.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments