Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys kwa magoli 5-4 dhidi ya Nigeria, leo waliingia uwanjani tena kucheza na Uganda ikiwa ni muendelezo wa kucheza michezo yao miwili iliyobaki ya makundi.
Kutokana na kupoteza mchezo wao wa kwanza Serengeti Boys walitakiwa kushinda michezo yote miwili ili wafuzu kucheza nusu fainali ya AFCON na kukata tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa nchini Brazil.
Bahati haikuwa yao Serengeti Boys ya mwaka huu kwani wamejikuta wakifanya vibaya zaidi ya wenzao waliokuwa wakishiki 2017 nchini Gabon, Serengeti Boys ya mwaka huu imepoteza kwa magoli 3-0 na ndoto za kukata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia 2019 nchini Brazil kuishia hapo.
Tunasema Serengeti Boys imetolewa kutokana na hata ikishinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Angola watakuwa na point 3 kitu ambacho hakitawawezesha kumaliza nafasi mbili za juu katika Kundi lao A, Serengeti Boys ya 2017 ilifanikiwa kupata point 4 katika michezo yake mitatu kutokana na kushinda mmoja na kutoka sare mmoja ila kupoteza kwao dhidi ya Niger dakika za mwisho ndio kumeua ndoto yao.
Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?