Baada ya golikipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga kumgomea kocha wake Maurizio Sarri kumfanyia mabadiliko wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la EFL dhidi ya Man City dakika ya 119, wengi walijuwa kuwa baada hapo ndio basi tena hatopata nafasi ya kucheza tena, kwani kitendo hicho ni cha utovu wa nidhamu.
Maurizio Sarri ameweka wazi kuwa kilichotokea kati yake na Kepa Arrizabalaga kimeshapita na maisha mengine yataendelea wala hakuna tatizo, kwa upande wa Chelsea mapema leo imetangaza kumkata mshahara wa wiki moja wa pound 190000 kama adhabu ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600, Kepa ambaye ni raia wa Hispania kwa sasa ana umri wa miaka 24 na alianzia soka lake katika club ya Athletic Bilbao ya Hispania.
“Baada ya tukio la jana kwangu jambo lile limeisha, ni mchezaji mdogo na amefanya makosa lakini basi na uhakika ametambua makosa yake, alifanya kosa kubwa sana lakini kwa upande wangu limesisha”>>> Maurizio Sarri
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake