AyoTV

Kauli ya Mwakinyo baada ya kumpiga Sinkala TKO round ya pili

on

Baada ya bondia Hassan Mwakinyo wiki iliyopita kumpiga bondia Said Azidu round ya kwanza sekunde ya 10 kwa TKO, usiku wa October 28 2018 Mwakinyo alirudi tena ulingoni kupigana dhidi ya bondia Joseph Sinkala katika pambano la round 10 la kuwania Ubingwa wa WBL na UBO, Mwakinyo alimpiga tena Sinkala round ya pili kwa TKO.

Pambano lilivyomalizika tu round ya pili na bondia Hassan Mwakinyo kupewa mikanda miwili ya WBL na UBO kwa ushindi huo, alipewa nafasi ya kuongea na mashabiki wake waliokuwepo uwanjani hapo kumsapoti, Mwakinyo ameendeleza rekodi yake ya kushinda pambano kwa TKO.

Angalia Mwakinyo alivyoendeleza ubabe, kampiga Sinkala TKO round ya pili

Soma na hizi

Tupia Comments