Michezo

Raheem Sterling kapokea tuzo ya heshima kwa heshima

on

Mshambualiji wa timu ya taifa ya England na club ya Man City ya England Raheem Sterling amepewa heshima ya (standing ovation) wakati akikabidhiwa tuzo ya heshima (The Integrity and Impact Award) ya BT Sport kwa kupiga vita ubaguzi wa rangi na kocha wake wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate.

Raheem Sterling ni miongoni mwa wachezaji ambao wamewahi kuktana na ubaguzi wa rangi lakini amekuwa imara kulipigania hilo, mwezi uliopita akiwa na timu ya taifa ya England katika mchezo wa ugenini dhidi ya Montenegro wakiwania kufuzu fainali za Euro 2020 Sterling, Danny Rose na Callum Hudson-Odoi waliitiwa kelele za nyani.

Kitendo cha kupokea tuzo au kuitwa mbele ya jukwaa kuzungumza wakati jina lako linatajwa huku watu wakisimama (standing ovation) kwa baadhi ya mataifa ikiwemo England huwa kinatafsirika kama ni heshima kubwa sana na kuonesha ishara ya kumuunga mkono.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments