Michezo

DONE DEAL: Chelsea wamemalizana na Borussia Dortmund

on

Club ya Chelsea leo imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa USA na club ya Borussia Dortmund Christian Pulisic kwa dau linalotajwa kufikia pound milioni 58, Pulisic ambaye alikuwa anwaniwa na Liverpool atajiunga na Chelsea mwisho wa msimu.

Christian Pulisic mwenye umri wa miaka 20 amekuwa ni miongoni mwa viungo mahiri wa Dortmund toka ajiunge na club hiyo mwaka 2015 akitokea PA Classic lakini akiichezea Dortmund game 115 na kupachika magoli 15, timu ya taifa ya USA akicheza game 20 na kufunga magoli 9.

Kiungo huyo atamalizia msimu akiwa na Borussia Dortmund wakati ambao Eden Hazard akiwa kabakiza miezi 12 katika mkataba wake na Chelsea, kwani bado anachelewa kufanya maamuzi kama ya kuendelea kusalia Stamford Bridge au kuondoka ila inaripotiwa kuwa atakuwa anasubiria ofa kutoka Real Madrid.

Kocha wa Simba baada ya kuwasili Zanzibar”Sio njia bora ya kuandaa timu”

Soma na hizi

Tupia Comments