Michezo

Pep Guardiola kashinda tuzo yake ya 7 EPL

on

Kocha wa Man City Pep Guardiola ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi April 2019 wa Ligi Kuu ya England wakati huu wakiwa mbioni kutetea taji lao la Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019, Guardiola ameiongoza Man City kushinda michezo yote mitano ya EPL ndani ya mwezi April.

Pep Guardiola amefanikiwa kushinda tuzo hiyo ya kocha bora wa mwezi April kwa mara ya pili msimu huu na kwa mara ya saba toka amejiunga na Man City 2016 kama kocha mkuu, ndani ya April amefanikiwa kushinda game mbili ngumu dhidi ya Man United Old Trafford na Tottenham katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad.

Man City ndani ya mwezi April game zao tano walizocheza ni game ya April 3 dhidi ya Cardiff City wakiwa nyumbani na kushinda 2-0, April 14 dhidi ya Crystal Palace na kushinda 3-1 ugenini, April 20 dhidi ya Tottenham 1-0 nyumbani, April 24 dhidi ya Man United na kushinda 2-0 ugenini na April  28 na Burnley nyumbani na kushinda 1-0.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments