Michezo

KRC Genk wanahitaji point 7 tu waandike historia na Samatta

on

Club ya KRC Genk ya Ubelgiji usiku wa April 27 2019 ilikuwa ugenini kucheza mchezo wake wa Play Off wa Ligi Kuu ya Ubelgiji dhidi ya KAA Gent, KRC Genk ndio vinara wa Ligi hiyo ambapo kwa sasa wamebakiza michezo minne na kazi kwao kujichanga kuhakikisha wanatwaaUbingwa.

KRC Genk wakiwa ugenini wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Leandro Trossard dakika ya 55, ushindi huo umewafanya KRC Genk waendelee kuongoza kwa kuwa na point 47 wakiwa wamecheza game 6 za Play Off na kubakisha nne huku wapinzani wao wakuu wakibakiza game tano wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 38 Club Brugge.

Ushindi hu0 sasa ili KRC Genk watangazwe kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji pasipokujali matokeo ya Club Brugge kama atafungwa au kushinda basi watahitaji point 7 watangazwe kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji Jupiter Pro, huku mtanzania Mbwana Samatta akiweka rekodi ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments