Michezo

Mbappe yuko radhi akae benchi Messi na Ronaldo wacheze

on

Mshambuliaji wa club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa na timu ya taifa ya Ufaransa Kyliane Mbappe ameonesha kuwakubali zaidi wakali wa soka Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa FC Barcelona, hiyo ni baada ya kuulizwa apange first eleven yake ni nani angemuweka benchi.

Mbappe kupitia jariba maarufu la michezo France Football aliulizwa swali kama akiwa katika timu na kuambiwa achague wachezaji wake wa kucheza nao katika Dream Team yake, kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi angempanga nani? Mbappe ameweka wazi kwa ubora wa wachezaji hao angewapanga wote na yeye kukaa benchi.

“Kama nikitakiwa kuchagua kuwa na kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika timu yangu? nitajiweka benchi mwenyewe ili wao wote waweze kucheza kwa sababu ni bora”>>> Kyliane Mbappe

Pamoja na kuwa Ronaldo na Messi bado wanatawala headlines za soka kutokana na ubora wao, Kyliane Mbappe ndio kinda anayetajwa kuja kung’ara na kutamba katika tuzo za Ballon d’Or kutokana na ubora wake ambao amekuwa akiuonesha, hivyo anatajwa kuwa baada ya utawala wa Messi na Ronaldo kumalizika anaweza kuwa yeye kwenye headlines.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments