Michezo

Yaya Toure kuhusu Bonucci kumbagua mchezaji mwenzake wa timu mmoja

on

Moja kati ya habari kubwa katika soka inayoenea kwa kasi ni kuhusiana na taarifa za kubaguliwa kwa mchezaji wa Juventus Moise Kean na mchezaji mwenzake Leonardo Bonucci, taarifa za kubaguliwa kwa mchezaji huyo zimekuwa gumzo kila kona katika mitandao.

Kutoka Kushoto ni Moise Kean na Leonardo Bonucci

Kitendo cha kubaguliwa kwa Moise kimekuwa gumzo kiasi cha kiungo wa zamani wa FC Barcelona na Man City Yaya Toure akizungumza na UEFA Equal Game kuweka wazi kuwa  kama angefanyiwa yeye na mchezaji mwenzake wa timu moja basi angemjua yeye ni nani

“Kwangu mimi ni nadharia mbaya kuwahi kukutokea katika mpira, mchezaji mwenzako anakushambulia kwa kusema vitu kama vile, unaweza kufikiria ingeniumiza kiasi gani wakati naona hivi vitu vikitokea tunatakiwa kufanya kitu ili kuendelea mbele haraka iwezekanavyo”>>> Yaya Toure

“Sitaki kuingia ndani zaidi kuhusiana na (Bonucci) alichokisema ni kumkosea heshima mchezaji mwenzake, sitaki kuwa mkali kuhusu yeye lakini angekuwa mchezaji mwenzangu mimi angenijua leo, anatakiwa kumuomba msamaha mchezaji mwenzake (Kean) na kuomba msamaha timu yake pia”>>> Yaya Toure

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments