Michezo

Gervinho kampa heshima swahiba wake DJ Arafat akiifunga Venezia

on

Staa wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye aliwahi kuichezea Arsenal Gervinho ameonesha heshima kwa rafiki na msanii DJ Arafat ambaye alifikwa na mauti August 12 2019 baada ya kupata ajali ya pikipiki, baada ya kupelekwa hospitalini DJ Arafat alipoteza maisha kutokana na kuumia sana.

Gervinho ameonesha heshima kwa DJ Arafat baada ya kuifungia goli club yake ya Parma ya Italia katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Venezia na kwenda kushangilia akiwa ameshika tisheti yenye jina na picha ya DJ Arafat kama heshima kwa staa huyo wa muziki wa Ivory Coast.

Mara kadhaa Gervinho na DJ Arafat enzi za uhai wake wamekuwa wakionekana pamoja, hiyo ni moja ya viashiria kuwa wawili hao walikuwa karibu ukizingatia wanatokea taifa moja,

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments