Mix

Baada ya Mbunge kuingia kila kona na Mabango Jimboni kwake

on

Wananchi wa kata ya Ruvu wamempongeza mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro kwa mtindo mpya aliokuja nao wa kutoa elimu kwa wananchi kwa kutumia mabango ambayo yanaonesha mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano katika Nyanja mbalimbali.

Wakizungumzia hatua hiyo ya mbunge kuelezea kazi zilizofanywa na serikali inayoongozwa na rais John Magufuli mmoja wa wananchi hao Jackson Duke na Ally Parasise wamesema ni ubunifu wa aina yake ambao haujawahi kufanywa na kiongozi mwingine katika jimbo hilo.

“Kwanza tunampenda rais wetu Magufuli na mbunge wetu kwa kuwa wanatuletea maendeleo lakini sasa amekuja na huu mtindo wa kutuelimisha kuhusu kazi ya Magufuli na serikali tunazidi kumpenda na tunaahidi hatutamuangusha”>>>Jackson

Walisema wana Imani kubwa na mbunge huyo kwa kuwa amekuwa akitekeleza ilani ya uchaguzi kwa kila anachoahidi lakini wakimpongeza Zaidi kwa mtindo wake wa kutatua kero za wananchi papo kwa papo.

“Hapa unaona anatekeleza ahadi alizoahidi lakini kuna shida mhe diwani kamueleza hapa hapa ametekeleza utapata wapi mbunge kama Mathayo “mwana wa kaya”>>> Parasise.

Akizungumzia mtindo huo mpya mbunge wa jimbo hilo Mathayo D.Mathayo amesema akiwa ni mbunge anaetokana na chama tawala anawajibika kumsaidia rais kuelezea wananchi mambo mazuri na makubwa yanayofanywa na serikali hivyo ya Rais John Magufuli kwa kutumia njia mbalimbali.

“Mhe Rais anafanyakazi kubwa na sisi kama wawakilishi wa wananchi na mhe Rais nimeona njia hii ni rahisi na inaeleweka kwa kuwa wananchi wanaona kile ambacho kimefanyika katika picha hivyo inawafanya wazidi kuelewa.”>>> DR Mathayo

Katika kata hiyo mhe Mathayo ametekeleza ilani kwa kukabidhi katika kata mifuko ya saruji,mabati,magodoro,fedha za kununua kinanda na fedha nyingine taslimu Zaidi ya shilingi  milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati,mabweni,na madarasa.

LIVE BUNGE: HUSSEIN BASHE ANAJIBU MASWALI

Soma na hizi

Tupia Comments