AyoTV

Rekodi mbili atakazoweka Samatta akicheza na kufunga goli UEFA Champions League

on

Leo UEFA Championsns League msimu wa 2019/2020 hatua ya makundi inaanza kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali, pamoja na kuwa Barcelona, Liverpool na Napoli zinacheza leo lakini watanzania wengi macho na masikio yao yatakuwa Austria kumtazama nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta atafanya nini?

Samatta akiwa na club yake ya KRC Genk ya Ubelgiji anakuwa Mtanzania wa kwanza kuwahi kucheza UEFA Champions League, Genk wakiwa ugenini kucheza dhidi ya Red Bull Salzburg (Sazibagi) nchini Austria.

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments