Michezo

Kaka wa Vidal aeleza kusikitishwa kwake mdogo wa kukosa muda wa kucheza Barcelona

on

Kaka wa mchezaji wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal anayeichezea FC Barcelona ya Hispania, amemtuhumu kocha mkuu wa timu ya FC Barcelona  Ernesto Valverde kutompa nafasi mdogo wake ya kucheza tofauti na alivyowasili katika club hiyo.

Kaka wa Vidal anayejulikana kwa jina la Sandrino ameonesha kusikitishwa na mdogo wake kukosa nafasi chini ya kocha Valverde msimu huu, Vidal hadi sasa hajaanza katika mchezo wowote zaidi ya kucheza kwa dakika 69 tu.

“(Vidal) hapati nafasi ya kucheza sana lakini siku zote nimekuwa nikijiamini na kumuunga mkono mdogo wangu, kocha amekuwa akibadilisha sana viungo , Arturo anastahili kupata muda wa kucheza lakini atapambana kwa sababu ni shujaa”>>> Sandrino

Valverde ameonekana kuwa na imani zaidi ya Frenkie De Jong, Arthur Melo na Sergio Busquets huku Arturo Vidal na Ivan Rakitic kuwa na wakati mgumu wa kucheza msimu huu, Valverde ameamua kufanya mabadiliko ya mfumo msimu ili kujaribu kuirudisha Barcelona katika ubora kitu ambacho kinamnyima nafasi Vidal na Rakitic.

VIDEO: Antonio Nugaz kaanza na Mbwembwe Yanga “Yanga unyonge kwisha”

Soma na hizi

Tupia Comments