Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys Oscar Mirambo, baada ya timu yake kupoteza mchezo wa kwanza wa fainali za AFCON U-17 dhidi ya Nigeria kwa magoli 5-4, amekiri kuwa game yao ya pili dhidi ya Uganda kesho itakuwa ngumu.
Oscar Mirambo ameeleza kuwa mchezo huo utakuwa na presha kubwa kwao kutokana na mchezo wao wa kwanza kupoteza, kwani ugumu wa mchezo wa kesho unakuja kutokana na timu hizo kukutana na Uganda ambayo imepoteza nao katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Angola kwa goli 1-0.
“Nimepata wakati wa kukaa na vijana kwa maana ya kuongea lakini pia kufanyika mazoezi japokuwa hauwezi ukafanya mazoezi ya nguvu sana wakati huu sio rafiki sana, hivyo kwa vyovyote vile tutataka kucheza na wachezaji bora tuliokuwa nao ambao pia tunaamini kuwa wanaweza wakafanya zaidi kama ambavyo wengine wanafanya ili mwisho wa siku tuweze kuhakikisha kuwa tunapata matokeo”>>> Oscar Mirambo
Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?