Siku 21 baada ya staa wa kimataifa wa Brazil aliyekuwa anaichezea FC Barcelona Neymar aamue kuihama club hiyo na kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa kwa rekodi ya dunia ya pound milioni 199, leo FC Barcelona wamesajili mbadala wake.
FC Barcelona ambao walikuwa wamelenga kumsajili mbrazil Philippe Coutinho kutoka Liverpool au Ousmane Dembélé kama chaguo lao la pili kama wakimkosa Coutinho, leo August 25 wamefanikiwa kumsajili Ousmane Dembélé kwa uhamisho wa pound milioni 96 ambazo zinaweza kuongezeka hadi kufikia pound milioni 136.
Kwa uhamisho huo sasa Ousmane Dembélé mwenye umri wa miaka 20 ndio anakuwa mchezaji wa pili ghali zaidi duniani baada ya Neymar, Dembele amesajiliwa akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani, maamuzi hayo ya FC Barcelona yamekuja baada ya kukataliwa kwa ofa yao ya tatu na Liverpool.
VIDEO: Penati ilizoipa Simba Ubingwa wa Ngao ya Hisani vs Yanga