Michezo

Refa aliyeipa penati Man United vs PSG ndio kapewa fainali ya Champions League

on

Baada ya utawala wa misimu mitatu mfululizo wa Real Madrid katika michuano ya UEFA Champions League, June 1 2019 tutapata nafasi ya kumshuhudia Bingwa Mpya kati ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Liverpool game ambayo itachezwa katika uwanja wa Wanda Metropolitano katika jiji la Madrid Hispania.

Kuelekea mchezo huo UEFA wamemtangaza muamuzi Damir Skomina kuwa ndio muamuzi wa kati wa mchezo huo ila hajawahi kucheza fainali ya Champions League hata mara moja, Dramir mwenye umri wa miaka 42 kutokea Slovenia aliingia katika headlines baada ya maamuzi yake ya game ya 16 bora kati ya PSG na Man United nchini Ufaransa kuinyonga PSG kwa kutoa penati dakika ya 94.

Pamoja na kuwa maamuzi hayo yaliitoa PSG katika game hiyo kwa kuipa Man United penati iliyopatikana kwa msaada wa VAR, bado uzoefu wa mechi kadhaa za Europa ikiwemo aliwahi kuchezesha fainali ya UEFA Europa League kati ya Ajax dhidi ya Man United  2017 na fainali ya Europa League na Super Cup kati ya Chelsea dhidi ya Atletico Madrid.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments