Michezo

Legend wa Man United anayeamini Paul Pogba atahama mwisho wa msimu

on

Imeripotiwa kuwa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Man United Paul Pogba kuna uwezekanao mkubwa wa staa huyo kutoendelea kuichezea Man United msimu ujao, kwa madai tetesi zinazoendelea kudai kuwa atahama club hiyo mwisho wa msimu zinaweza kutimia.

Moja kati ya watu wanaozipa nguvu taarifa hizo ni staa wa zamani wa Man United Paul Ince, kwani pamoja na kuwa Paul Pogba kiwango chake kimeimarika chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer ukilinganisha na hali yake ilivyokuwa chini ya Jose Mourinho, anaamini kuwa anaweza kwenda kujiunga na Real Madrid.

“Namuamini Paul Pogba, Ole anatakiwa kumshawishi kubakia (Man United) anaweza kuitengeneza timu kumzunguuka yeye kuelekea kwa washambuliaji, hilo ni kama (Ole) anataka (Pogba) abakie Man United, kiuweli sifikirii kama Paul Pogba atabakia Old Trafford msimu ujao”>>>Paul Ince

Paul Ince ambaye aliwahi kucheza Man United kwa miaka 6 (1989-1995) ameweka wazi kuwa kitakuwa sio kitu kizuri kama Man United hawatomaliza TOP 4 msimu huu, Paul Ince kwa sasa ana umri wa miaka 51 lakini ni moja kati ya wachezaji wenye heshima sana katika club ya Man United.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments