Habari za Mastaa

Calisah anunuliwa gari na aliekuwa mapenzini na Otile Brown, Vera Sidika

on

Kumekuwa na tetesi kuwa Mwanamitindo Calisah amekwea pipa mpaka +254 nchini Kenya na kumrithi muimbaji Otile Brown chombo alichokuwa akikimiliki hii ni baada ya Vera Sidika na Otile Brown kuachana rasmi wiki kadhaa zilizopita.

Calisah ameonekana kuanzisha penzi jipya na Mwanadada huyo Vera Sidika ingawa alikanusha taarifa hizo kwenye kipindi cha Clouds Fm cha Uheard na Soudy Brown na kusema kuwa yupo tu nchini humo kwaajili ya kazi .

Leo November 7,2018 Penzi hilo linaonekana kukolea kati ya wawili hao na hii ni baada ya Vera Sidika kutumia ukurasa wake wa instagram kupost picha inayoonyesha kuwa amemnunulia Calisah gari aina ya Mercedez Benz na kuandika “Huwa natimiza aahadi siku zote, natumaini umependa gari lako jipya”

Wema “Ninaumwa sana na bado sijapona ila sitohudhuria hayo maombi”

Soma na hizi

Tupia Comments