Michezo

Waziri Bashungwa kumuenzi hayati baba wa Taifa katika mbio za riadha

on

October 14 2019 kumbukumbu ya siku ya kifo cha baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere, taasisi mbalimbali Tanzania huwa wanamkumbuka Nyerere Day kwa namna yake lakini Atlas School wameandaa mbio za riadha maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa.

Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Atlas Sylvanus Rugambwa

Mbio hizo zitafanyika na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa atakuwa mgeni rasmi katika mbio hizo zitakazofanyika Madale jijini Dar es Salaam, Waziri Bashungwa atashiriki pia mbio za marathon za 21 KM.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Atlas Sylvanus Rugambwa ameeleza kuwa mbio hizo kwa mwaka huu zitashirikisha jumla ya washiriki 2000, nje ya mbio za kilometa 21 pia kutakuwa na mbio za 5KM na 10KM hata hivyo pia mbio hizo zina lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa maktaba ya umma.

VIDEO: Salim Kikeke kafunguka makubaliano yake na MO Dewji ubalozi wa Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments