Michezo

Picha 21 za jinsi Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo alivyomshughulikia Muargentina

on

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo leo March 23 2019 alikuwa Nairobi Kenya kupambana na Bondia wa kimataifa kutokea Argentina Sergio Gonzalez ambaye anatokea kwenye moja ya mataifa yenye nguvu duniani kwenye michezo.

Pamoja na kuwa Gonzalez alikuwa anatokea taifa lenye nguvu kimichezo hiyo haikumtisha wala kumfanya Mwakinyo kumuogopa au ashindwe kumpiga, kafanya kweli na kumpiga round ya 5 kwa Technical Knock Out (TKO).

Kabla ya pambano hili Mwakinyo aliweka kambi Liverpool Uingereza kwa ajili ya maandalizi akifundishwa na Tony Bellew, ni maandalizi ambayo yameonekana kumsaidia kumpa ushindi wa leo.

ULIPITWA NA MC PILIPILI???? ASEMA “NIMEZOEA KUZINGULIWA KWENYE MAPENZI, NI SHETANI… SIKUWAHI KUPATA MZURI KAMA HUYU” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments