Wakati kukukiwa na tuhuma mbalimbali kuhusiana na aliyekuwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir baada ya kupinduliwa, ameendelea kufanyiwa uchunguzi ili kuweza kubaini mambo mbalimbali yanayomuhusu kiongozi huyo kabla ya kushitakiwa.
Omar al-Bashir leo ameingia katika kashfa mpya baada ya askari wa Sudan wanaoendelea na uchunguzi dhidi yake, kubaini kuwa alikuwa amejilimbikizia kiasi kikubwa cha pesa kinyume na sheria, leo Omar al-Bahsir ambaye yupo chini ya ungalizi zimekutwa zaidi ya Tsh Bilioni 300 nyumbani kwake.
Katika uchunguzi huo ambao ulibaini kuwepo na fedha katika mifumo ya viroba, ulikuta kiasi cha pesa kwa noti mbalimbali, fedha zilizokutwa katika nyumba ya Omar al-Bashir ambazo jumla yake zina thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 300 ni dola za kimarekani 351000, euro milioni 6 pamoja na pound bilioni 5 pesa za kisudan.
Omar al-Bashir pamoja na kuwa na tuhuma mbalimbali lakini kukutwa na pesa hizo kutamfanya afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa, taarifa za kuondolewa madarakani kwa Rais huyo ziliripotiwa April 11 kisa kikiwa ni shinikizo la wananchi kutokana na hali ya maisha na uchumi wa nchi hiyo kuwa mgumu, Omar al-Bashir alikuwa Rais wa 7 wa Sudan na alikuwa madarakani kuanzi 1989-2019 sawa na kutawala kwa miaka 30.
“Siwezi kusubiri Rais Magufuli anitumbue mimi”-Naibu Waziri Masauni