Michezo

Smalling kaigharimu Man United, presha ya TOP 4 inazidi kupanda

on

Club ya Man United imerudi katika wakati mgumu kufuatia kupoteza kwa mchezo wake wa 32 wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Wolves, Man United wakiwa ugenini wamejikuta wakipoteza kwa magoli 2-1, licha ya kuwa matokeo hayo hayakutarajiwa na wengi.

Young akioneshwa kadi nyekundu na muamuzi Mike Dean dakika ya 57, kadi hiyo imemfanya Mike Dean kuwa kocha wa kwanza EPL kufikisha jumla ya kadi nyekundu 100.

 

Kipigo hicho kwa magoli ya Diogo Jota dakika ya 25 na beki wa Man United Chriss Smalling kujifunga dakika ya 77, huku timu ikiambulia goli moja lililofungwa mapema na Mctominay dakika ya 13, wameanza kuwa katika presha ya kuipoteza nafasi ya TOP 4 ambayo itawapa tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 ila kwa bahati mbaya kipigo kinawaweka nafasi ya 5.

Smalling akijifunga dhidi ya Wolves

Msimamo wa Ligi Kuu kwa sasa unaonesha nafasi ya tatu, nne na tano ndio wanagombania Arsenal, Tottenham na Man United ila mmoja kati yao atabidi amalize nje ya TOP 4 kama hatokuwa makini wakati Liverpool na Man City wakiwa kileleni huku wakiviziana nani ateleze amuachie mwenzake taji.

Man United nafasi ya 5 point 61 kama Tottenham ila Man United ameizidi Tottenham mchezo mmoja zaidi.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments