AyoTV

VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6

on

Golikipa wa Juma Kaseja leo Jumapili ya July 28 2019 ameandika historia mpya katika soka lake kufuatia kurudi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa mara ya kwanza baada ya miaka 6, Kaseja mara ya mwisho kuichezea Taifa Stars ilikuwa 2013 na mara ya kwanza ilikuwa ni 2002, leo amerudi ana nini cha kusema.

“Namshukuru Mungu kwa sababu alipangalo Mungu hakuna binadamu anayeweza kulipangua, nilitoka timu ya taifa lakini muda wote waliokuwa wanacheza ni watanzania kama mimi na mimi leo nimerudi ni mtanzania mimi nadhani tuungane tuipiganie nchi yetu”>>>Juma Kaseja

Baada ya mchezo wa leo wa Tanzania kuwania kucheza CHAN 2020 kumalizika kwa sare tasa 0-0, sasa Taifa Stars itakuwa na safari ya kwenda Kenya kucheza mchezo wa marudiano August 4 huku wakihitajika kupata sare ya 1-1 au ushindi ili kusonga hatua inayofuata.

KOCHA TAIFA STARS “HUO UZOEFU ATAUPATA WAPI? NI MTANZANIA ANA HAKI”

 

Soma na hizi

Tupia Comments