Ndoa ya Kocha wa klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza na mke wake ,Cristina Serra Imevunjika rasmi baada ya kudumu kwa muda wa miaka 30.
Guardiola na mke wake wamekuwa wakiishi tofauti kwa muda wa miaka mitano huku Guardiola akiendelea na kazi zake huko Manchester city na mke wake akifanya kazi zake za mitindo huko Barcelona.
Wawili hao walikutana Toka wakiwa na umri wa miaka 18 na kufunga ndoa mwaka 2014,huku wakibahatika kupata watoto watatu mabinti wawili wenye umri wa miaka 24 na 17 huku mtoto wakiume akiwa na umri wa miaka 22.
“Mke wangu ndiye bora zaidi ulimwenguni kwa vitu vingi, lakini haswa katika mitindo” Guardiola kwenye moja ya mahojiano