Mix

RC Makonda kuhusu agizo alilodaiwa kulitoa la wakamatwe wanaolala Guest

on

Hivi karibuni kumekuwa na headlines zinazomuhusisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu kutoa agizo la wanaolala kwenye nyumba za wageni wakamatwe hasa nyakati za mchana.

Sasa millardayo.com & Ayo TV imempata RC Paul Makonda na kuyaongea haya>>>>Hili suala mimi nimelisikia moja aliyetoa maelezo anasema nina umbea maana yake kwanza ni mmbea, Serikali haijawahi kufanya kazi kwa namna hii na wala hakuna maelekezo ya namna hiyo’

Lakini la pili kufahamu ambalo ni jambo jema ni kwamba kabla ya kufanya maamuzi ya kuandika habari au kutangaza habari ni vema pia ukaonana na mamlaka husika anasema Polisi maana yake lazima kamanda Sirro aulizwe na atoe taarifa Je ni kweli kuna taarifa kama hizo’

‘Ukweli ni kwamba hakuna maelekezo ya namna hiyo, wapo watu wanatoka maeneo mbalimbali wanakuja Dar es Salaam katika nyumba za wageni kupumzika, wapo watu wanaingia usiku wa manene na ndio maana kukawa na nyumba za wageni ‘

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza RC Paul Makonda akizungumzia agizo alilodaiwa kutoa la wakamatwa wanaolala Guest

ULIKOSA ALICHOKIONGEA WAZIRI MKUU MAJALIWA KUHUSU WAHUSIKA WA MAUAJI YA ASKARI BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments