Mix

Watalii wanapojikuta na hatia kwa kesi ya kuvua nguo juu ya Mlima !!

on

478

Kuna wakati watu wengine sio kwamba hawapendi watalii au hawapendi utalii kwenye nchi yao, Utalii unakuja na vingi ikiwemo utamaduni mgeni.. Ukiwa maeneo ya Beach hivi kukutana na Watalii wakiwa na nguo ndogondogo huku wakipunga upepo ni kawaida tu, lakini kwa wengine hiyo sio sawa!!

Watalii wanne wamejikuta wakiingia kwenye Headlines za vyombo vikubwa vya Habari Duniani kama Sky News, BBC na CNN.. ishu ni kitendo cha Watalii hao kuvua nguo wakati wanatalii juu ya Mlima Kinabalu ulioko Malaysia, alafu wakapiga picha wakiwa hawajavaa nguo kabisa !!

Mwongozaji wa Watalii hao aliwaambia lakini kwamba ishu ya kuvua nguo sio poa kabisa kwa Malaysia na Sheria zao, majibu yao hayakuwa mazuri>>> “shut up” and “go to hell“.

Jamaa hao walianza kama utani yani kutaniana nani ataweza kuvua nguo alafu wapige picha, matokeo yake wote wanne wakavua.. Mitandao ikakuza story mwisho wake kesi yao inaendelea Mahakamani.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments