Duniani

Kama kuna hukumu za kushtua iko na hii, miaka 885 jela !! Kisa..? Stori na video yake..

on

Najua tumeshawahi kukutana na stori kuhusu hukumu za kifungo cha miaka kadhaa mpaka 30 jela, au wengine wanahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kufanya makosa mbalimbali… lakini kuna hukumu ambazo ukitajiwa namba za miaka yake unaona bora kama hukumu yenyewe ingekuwa tu kifungo cha maisha !! Miaka 885 jela, anatoka mtu kweli hapo ?!

Shawn Ryan Thomas alidakwa na Polisi Florida Marekani akiwa na picha za utupu za watoto wadogo, kesi ikafika Mahakamani na hukumu yake ikatolewa kwamba atatakiwa kutumikia jumla ya miaka 885 jela.

Shawn_Ryan_ThomasNEW

Ripoti nyingine kutoka  Florida Department of Law Enforcement imesema Thomas alinaswa pia akiwa kwenye mpango wa kumteka msichana mwingine mdogo, kuwaua wazazi wake na kumrekodi mkanda wa utupu !!

Stori yake iko kwenye Video pia mpaka Mahakama ilivyomsomea hukumu.

https://www.youtube.com/watch?v=GNrYNJvFKZc

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments