Wabunge wa Senegal wamerushiana makonde Bungeni, mzozo huu unajiri huku kukiwa na uhasama kati ya Wanasiasa wa Chama Tawala na Upinzani.
Tukio hilo lilitokea wakati wa upigaji kura kuhusu bajeti ya Wizara ya Sheria ya mwaka ujao.
Katikati ya uwasilishaji wa Bajeti, Mbunge wa Upinzani Massata Samb alimpiga Amy Ndiaye Gniby wa Muungano Tawala wa Benno Bokk Yakaar (BBY).
Gniby alilipiza kwa kurusha kiti upande wa Samb kabla ya Mbunge mwingine kumvuta hadi sakafuni na hatimaye kikao hicho kilisitishwa huku Wabunge wakiendelea kurushiana makonde na matusi.
View this post on Instagram